Takribani watu 35 hivi sasa imethibitishwa kuwa wameuwawa katika mapigano kati ya jeshi la Burundi na kundi la waasi lisilojulikana karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Afisa mmoja mwandamizi wa jeshi la Burundi ameliambia shirika la habari la AFP leo hii kwamba hadi sasa wamepata maiti 34 za washambuliaji na kwamba wamempoteza mwanajeshi mmoja kwa upande wao, ikiwa ni siku moja baada ya kundi hilo la waasi kuishambulia nchi hiyo ya Afrika ya kati. Ameongeza kusema kwamba vikosi vya usalama bado vinafanya msako kwenye eneo yalipozuka mapigano hayo na kwenye mabonde wanakojificha waasi hao. Hata hivyo wakaazi kadhaa wa eneo hilo wamesema wanaamini kwamba idadi ya maafa kwa upande wa serikali ilikuwa kubwa ambapo imeripotiwa kwamba sio chini ya wanajeshi watano wameuwawa. Imeripotiwa kwamba waasi 200 walivuka mpaka na kuingia mkoa wa Cibitoke kaskazini mwa mji mkuu wa Bujumbura wakati wa usiku hapo Jumatatu.
31 Desemba 2014 - 19:33
Msimbo wa Habari: 661916
Takribani watu 35 hivi sasa imethibitishwa kuwa wameuwawa katika mapigano kati ya jeshi la Burundi na kundi la waasi lisilojulikana karibu na mpaka wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.